Friday 17 October 2014

NAJUTA MIE YA NIVA NI FUNDISHO KWA VIJANA WANAOPENDA KULELEWA NA MAJIMAMA

Filamu ya Najuta mie ya msanii mwenye jina kubwa nchini Niva Zuberi imeonekana kuwa fundisho kwa vijana wanaopenda kulelewa na wa mama wenye pesa zao badala ya kujituma kufanya kazi kwa bidii

Akifunguka kiafrika bila hofu yoyote kwa kuwa Tanzania ni nchi huru niva amesema filamu hiyo ameitoa baada ya kuona vijana wengi wanapenda maisha rahisi na kushindwa kufanya kazi badala yake wanaishia kumtegemea mwanamke bila kujua mwisho wake ni mbaya

Kwenye filamu hiyo ambayo ni gumzo kwa hivi sasa nchini Niva ameonesha uwezo mkubwa wakuongea rafudhi ya mtu aliewai kuishi Marekani uku akitumia jina la Mario.

Pia ameweza kuwashirikisha wasanii wengi waliowai kujipatia umaharufu kupitia tamthilia ya jumba la dhahabu
wasanii hao ni Nikita pamoja na Mam tea  ambao wameonesha uwezo mkubwa sana kwenye filamu hiyo inayosukumwa nchini na kampuni ya steps entertainment jipatie nakala yako uone kilichoonekana ndani

No comments:

Post a Comment