Friday 31 October 2014

DAVINA: BONGO MOVIE HAIJANIPA MUME

MSANII wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’ amesema wanaomsimanga kuwa amepata mume kwa sababu yao hawana hoja kwa sababu Bongo Movie Unity haina ubavu huo.

“Mimi sijatafutiwa mume na Bongo Movie, alinitafuta mwenyewe baada ya kuniona kwenye muvi yangu ya Tone la Damu akiwa Italia, sasa nashangaa na ninaumia ninaposikia eti Bongo Movie walinitafutia.
“Ukweli naombeni mniache kwa sababu hakuna aliyehusika kwa kitu chochote kunikutanisha na mume wangu, hivyo acheni kunisengenya na mimi siringi kwa chochote kama ni kutoka huko kwenye kundi ni maamuzi yangu maana sikuwa naona faida yoyote,” alisema Davina.

No comments:

Post a Comment