Thursday 23 October 2014

‘UKAWA’ YAZALIWA BONGO MOVIE

WASANII wa filamu ambao hivi karibuni waliripotiwa kujitoa katika kundi la Bongo Movie Unity wamedaiwa kuunda la kwao linalojulikana kama Ukawa ambalo litakuwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti aliyetimuliwa, Steven Mengere maarufu kama Steve Nyerere.

Baadhi ya wasanii wanaotajwa kuunda kundi hilo kwa mujibu wa chanzo chetu makini ni pamoja na Devotha Mbaga, Salama Salmin ‘Sandra’, Halima Yahya ‘Davina’ na wengineo.
“Yaani sasa hivi haya makundi mawili kuna vita kali sana, kila moja linataka lionekane kwamba lina nguvu kuliko lingine, hata jina la Bongo Movie Unity limebadilishwa sasa hivi linaitwa Bongo Movie Stars

Mussa Issa ‘Cloud’ alikiri kubadilishwa jina kwa Bongo Movie Unity na pia amesikia habari za kuwepo kwa kundi la Ukawa wakati Steve Nyerere alisisitiza kuwa bado ni mwanachama wa Bongo Movie Unity na kwamba mtu anayetaka kuwagombanisha wasanii anajulikana.

No comments:

Post a Comment